Upishi wa maandazi ya nazi na zabibu kavu.

Vifaa:

  1. Unga wa ngano
  2. Mafuta ya kula au Samli
  3. Hiliki
  4. Zabibu kavu
  5. Nazi
  6. Maji
  7. Chumvi
  8. Sukari
  9. Hamira ya chenga.
  10. Vanilla flavor

Matayarisho:

  1. Weka unga wa ngano kwenye chombo cha kukandia, tia hamira ya chenga, chumvi kidogo, hiliki, vanilla, zabibu kavu, sukari na samli au mafuta ya kula kisha anza kuchanganya.
  2. Ukishachanganya anza kuweka tui la nazi kidogo kidogo huku unakanda, kama unaona unga ni mgumu tia maji huku ukiendelea kukanda.
  3. Unga ukishakua laini (usiwe laini sana wala mgumu sana) anza kukata madonge kama ya chapati.
  4. Ukishamaliza sukuma donge moja kwenye kibao cha chapati kisha katakata kwa size na style upendayo.
  5. Ukishamaliza acha maandazi yaumuke. (Yaache kwa nusu saa).
  6. Weka kikaango jikoni, mimina mafuta ya kula, weka moto wa wastani kisha anza kuchoma maandazi.
  7. Yakianza kubadilika rangi kwenda ya brown geuza upande wa pili. Yakiiva toa jikoni, chuja mafuta kwa ajili ya kula.

Leave a comment