Upishi wa Visheti

Vifaa:

1. Unga wa ngano

2. Baking Powder

3. Siagi

4. Vanilla

5. Icing sugar

6. Maziwa ya maji

7. Nazi

8. Mayai

Matayarisho:

1. Kuna nazi halafu isage kwenye blender.

2. Changanya unga wa ngano na baking powder.

3. Changanya siagi kwenye unga, weka nazi uliyosaga, vanila na mayai.

4. Anza kutia maziwa kidogo kidogo huku ukiwa unakanda mchanganyiko kama unga wa chapati.

5. Sukuma kama muundo wa chapati na ukate vipande vidogo vidogo.

6. Weka karai jikoni na mafuta kwa ajili ya kukaanga (weka moto wa kiasi)

7. Ukimaliza kukaanga, viweke katika bakuli uchanganye na ice and sugar wakati visheti vikiwa bado vya moto.

Asanteni.

Naomba acha comments na maoni yenu.

One Comment Add yours

  1. Fadhila says:

    Asante sana nimefanya kama ulivyoelekeza vitamu balaa

    Like

Leave a comment